Matibabu ya kisheria, Dua mbalimbali na dawa za kisunna

Matibabu ya kisheria, Dua mbalimbali na dawa za kisunna

Karibu

Dua mbalimbali

Qur'an

Qur'an

Dua za kuomba riziki

Assalam alaikum warahamatullah wabarakatuh.

Sifa zote njema ni zake Allah, mwenye kujibu maombi ya mwenye kumuomba pale anapo muomba, na sala na salam zimfikie mtume Muhammad na Ali zake na sahaba zake na wale wote walio ifuata njia Yao mpaka siku ya mwisho.

Ukurasa huu ni maalum kwa ajili ya Dua mbalimbali ambazo tunapaswa kuomba sisi waislamu kwa Allah subhannallah wa taallah kwenye hali mbalimbali.

Kwa kuanzia hapa tutaleta Dua kadhaa za kuomba milango ya riziki kufunguka, dua hizi miongoni mwazo zimetoka kwenye Qur'an tukufu na sunna, miongoni mwetu tumekuwa tunaomba Dua lakini hatupati majibu,  sababu kubwa ni kwamba hatuelewi adabu na vizuizi vya dua kujibiwa haraka na zinazofungua milango ya riziki.

Kabla hatujaenda moja kwa moja kwenye Dua ambazo tukiomba zinakuwa ni sababu ya kufunguliwa milango ya riziki, awali tutambue sababu za kufungua milango hiyo ya riziki kwani usipozifahamu na kuzifuata huenda ikawa kuzisoma Dua hizo ni kazi bure au kupata faida kidogo. 

*Kufunga undugu na nakuwatendea wema wazazi wawili.

*Kuzidisha kumuomba Allah msamahama kwa madhambi tunayofanya.

Swala za haja, kabla ya kusali Sala za haja tunapaswa tutawadhe udhu sahihi, Kisha tujisitiri mwili, na tutekeleze nguzo zake na wajibu wake, Kisha nia moyoni kwa  haja tunayokusudia.

 

Sala ya haja ina rakaa mbili, baada ya kusali raka mbili hizi mja anatakiwa kujinyenyekeza na kujidhalilisha kwa Allah ili Allah amkidhie haja yake inayo mtatiza, au kumuomba Allah juu ya jambo linalompa tabu limuondokee.

Hakuna wakati maalum wa Sala ya haja, lakini kuna nyakati bora zinazotarajiwa Dua kujibiwa, nazo ni baada ya adhana, usiku wa manane nakadhalika.

Lakini pia ukurasa huu utawahusu Waislam na wasio Waislam tuwasiliane kwa kupitia njia hizi za mawasilino.

Dua ya kwanza. 

اللهم فارج اهم وكاشف الغم مجيب دعوة المضطرين رحنا ما لدنيا والأخرت ورحيمهما إرجمني رحمة تعتني بها عن رحمة من سواك 

Allahumma faarijal hammin wa kaashifal ghammi mujiiba  da'wati  l mudh tariina rahamaanaddunin ya Wal akhiratul warahiimahumaa irhamni rahimiin tughninii bila an rahmatin man siwaaka.

Dua ya pili 

((اللهم ا كغني بحلالك عن كرامة واغنني بفضلك عمن سواك))

Allahumma akfini bihalalika an haramika wa bifadhilika Amman siwak. 

Dua ya tatu 

ربنا آتنا في دنيا حسنة وفي آخرة حسنة وفيما عذاب)) ((النار 

Rabbanaa aatinaa fidduniyaq hasanah wafil aakhirati hasanah waqinaa adhaabannar.

Tutaendelea kuleta mtiririko wa Dua mbalimbali kwenye ukurusa huu In Sha Allah.

Ayatul kifaayat, hapa hatuna lolote miongoni mwa vita ya kimadhehebu ila ni kuzingatia kuwa Allah amejalia Qur'an yote kuwa ni sehemu ya utatuzi wa maradhi kimwili na kiroho (ponyo) na rehema kwa kila jambo, iwe elimu, biashara, sayansi, zaka, funga, hija, ndoa, adabu, familia, watoto nakadhalia ((kama ambayo ni vigumu mja kuorodhesha yote hata akipewa miaka na miaka kufanya kazi hiyo, Allah amesema, hata bahari ikiwa wino wa kueleza sifa zake bahari hiyo itaisha na ikiongeza nyingine itaisha hali ya kuwa bado sifa za Allah hazijaisha na zinahitaji bado kuelezwa)) Allahu ya alam.

Ayatul kifaayat, hapa hatuna lolote miongoni mwa vita ya kimadhehebu ila ni kuzingatia kuwa Allah amejalia Qur'an yote kuwa ni sehemu ya utatuzi wa maradhi kimwili na kiroho (ponyo) na rehema kwa kila jambo, iwe elimu, biashara, sayansi, zaka, funga, hija, ndoa, adabu, familia, watoto nakadhalia ((kama ambayo ni vigumu mja kuorodhesha yote hata akipewa miaka na miaka kufanya kazi hiyo, Allah amesema, hata bahari ikiwa wino wa kueleza sifa zake bahari hiyo itaisha na ikiongeza nyingine itaisha hali ya kuwa bado sifa za Allah hazijaisha na zinahitaji bado kuelezwa)) Allahu ya alam.

Miongoni mwa dua za kuomba rizk

Assalam alaikum warahamatullah wabarakatuh

Sifa njema ni za Allah, mwenye kujibu maombi ya mwenye kumuomba pale anapo muomba, na sala na salamu zimfikie mtume wake na ali zake na sahaba zake na wale walio ifuata njia Yao mpaka siku ya malipo.

Ama, kwenye ukurasa huu kama tulivyosema mwanzo tutaleta Dua mbalimbali, lakini pia tulieleza mambo muhimu ya wajibu kwa muislam kuyafuata ili dua zijibiwe na si tu kujibiwa bali kwa urahisi lakini si sehemu ila kwa ukamilifu kama alivyotarajia.

Leo tupate elimu kwa kadiri Allah atakavyokuwa amejalia juu Aya miongoni mwa ayya ziitwazo " ayatul kifaayat" wenye elimu wameorodhesha kwa idadi, hapa hatuta elezea idadi ya Aya hizi ila tueleza baadhi ya Aya hizi tukufu biidhinillah Karim.

Yako mengi ya manufaa ambayo wajuzi wameainisha kuwa kwa kutumia Aya hizi dhiki, madhila, haja kubwa na ndogo kwa jaalah zake Allah subhannahu wa taallah mja akiwa kwenye tabia njema ya kumuomba Allah basi hupata muradi wake.

Aya hizi kama ambavyo tunavyoelewa sasa Qur'an nzima ni Rukya basi Aya hizi pia ni sehemu ya Qur'an Allah subhannahu wa taallah ameweka ndani ya hizi Aya ponyo na Rehema kwa haja mbalimbali. Iwe ni maradhi au shida mbalimbali.

Aya hizi kama zitasomwa kwa imani na adabu, na kuzingatia sheria za kumuomba Allah kwa idhini yake Allah tunasaidika kwa mambo mengi mno, hapa tufahamu machache yafuatayo:

*Kutibu baadhi ya maradhi.

*Kuondoa matatizo na kupata suluhu ya mabalaa mazito madeni, migongano na migogoro, kudhulumiwa, kesi, majini na uchawi.

* Uislam aukatizi mtu kuwa tajiri ispokuwa kwa njia ya haki ya Allah, basi Aya hizi husaidia pia kama mja anataka kuwa na utajiri na akadumu kumuomba Allah kupitia Aya hizi kwa Nia dhabiti na na imani kubwa.

* Kusaidia kuondoa jeuri na kiburi cha wenye mamlaka wasio na haki kufanya hayo.

*Msafiri kufika salama kwenye safari yake.

* Kutafuta kazi. 

* Kuondoa nuksi.

*Ulinzi dhidi ya majambazi na uchawi na kadhalika.

Kwenye maradhi ya aina yoyote basi Aya hizi zisomwe mara Saba Kisha mgonjwa atapuliziwa mwili mzima shida na madhila yatapungua kwa kiasi kikubwa.

Kwa riziki ya utajiri mja asome Kila baada ya Sala ya faradhi mara sabini. Au kwa siku mara mia tatu na hamsini, ataona maajabu ya kadiri Mali zinavyo kusanyika, hapa nitoe angalize sio sasa mja akae tu bila kufanya kazi yoyote hapana lazima kuwe na amali, mja afanye kazi na kupitia kazi hiyo au kazi hizi basi Allah ataremsha Rehema zako na mja atapat muradi wake Allah ya alam.

Kuomba jambo lolote ka heri, basi mja ataswali rakaa mbili za sunnatil haja, baada ya hapo Kisha atakaa kitako na kukariri Dua hii mara 41, na Kisha Alam na sh rah 41, In Sha Allah atajibiwa ombi lake.

Kama mja kwenye biashara yake kuna uzito mkubwa, biashara imefungika na hakuna wateja ili biashara ifunguke basi akiwa kwenye hali ya udhu asome Aya hizi mara 41 in Sha Allah biidhinillah biashara hiyo itafunguka na wajeta watafika na kuongezeka, zingati bidhaa ziwe kwenye unora na mazingira safi na haki kwenye kuuza.

Kuondoa mabalaa, nuksi na mikosi Aya hizi zisomwe kwenye maji mara 99 kisha oge mja hayo yaliyosomewa, atafanya hivyo kwa muda wa siku saba, Allah atajalia hali hizo zitaondoka, na atafanya hivyo kwa muda siku saba lakini pia atapaswa kuoga nje ya choo au bafu, sehemu iliyofichika na sio kuoga majiani au sehemu iliyo wazi, aoge akiwa anavazi juu sio kuoga pekupeku, ataoga kwa kutanguliza dua ili Allah amlinde na mashetani.

Somo hili linaendelea....





X
This site uses cookies to offer you a better browsing experience.
You can accept them all, or choose the kinds of cookies you are happy to allow.
Privacy settings
Choose which cookies you wish to allow while you browse this website. Please note that some cookies cannot be turned off, because without them the website would not function.
Essential
To prevent spam this site uses Google Recaptcha in its contact forms.

This site may also use cookies for ecommerce and payment systems which are essential for the website to function properly.
Google Services
This site uses cookies from Google to access data such as the pages you visit and your IP address. Google services on this website may include:

- Google Maps
- Google Fonts
Data Driven
This site may use cookies to record visitor behavior, monitor ad conversions, and create audiences, including from:

- Google Analytics
- Google Ads conversion tracking
- Facebook (Meta Pixel)