Mafundisho
Namna bora ya kujilinda kwa Allah dhidi ya masheitwani na uchawi.
Assalam alaikum warahamatullah wabarakatuh
Kwahakika Allah subhannallah wa taallah ametulinda Waja wake dhidi ya vitimbi na madhila ya viumbe alivyoviumba na Kwa kuvikadiria umbali kati Yao na sisi, na kama madhara yatokanavyo kwavyo hutufika pale anaporuhusu kitufika kwa namba aliyopanga yeye.
Allah amejalia njia imara kwetu kwa kujilinda dhidi ya Shari za viumbe haya, kupitia mtume wake Muhammad swallahu alaihi wa salaam tumepata mafunzo mbali mbali ya jinsi ya kujilinda kwa kujisalimisha kwake Allah dhidi ya Shari za viumbe na Shari za nafsi zetu. Zipo Aya na sura kwenye Qur'an maalum kwa ajili ya kutafuta hifadhi kwa Allah subhannah wa taallah, lakini zipo Azkar nyingi mno ambazo pamoja na aya na sura hizi mja huwa anakuwa kwenye ngome kubwa.
Lakini kutokana namafunzo haya pia kuna taratibu za kufuata ili kuwa salama salmon taratibu hizi, ni kuwa na udhu kwa kurudisha Kila unapotenguka, kulala na udhu, Dua wakati wa jimai, kuhifadhi swala, kusoma Qur'an ndani ya nyumba, kuondoa midoli ndani ya nyumba, kuondoa muziki, kusoma Qur'an, lakini kwa maalum suratul Bakarah walau mara Moja kwa wiki, kuzungumza kwa sauti ya chini ndani na nje ya nyumba, kusema Bismillah Rahman Rahim linapoanzwa jambo la kheri, kusema Bismillah Rahman Rahim wakati wa kula, kukaa chini pindi unapopatwa na hasira(hii husaidia kurudisha hasira chini, na mtume wa Allah ameainisha hali kadhaa mabapo majini humvaa mja au uchawi kungia mwili mwa mja, Moja ya hali hizi ni wakati maja anapokuwa na hasira) lakini kuna Azkar za asubuhi na jioni, hizi zinatakiwa kusomwa asubuhi na jioni Kila siku.
Niwasihi nyote, tujitahidi kutenga muda wa kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na elimu ya dini walau kwa wiki masaa matatu.
Usisite kuwasiliana nasi kupitia namba ya simu au barua pepe ili upate mfumo mzuri na rahisi kujifunza kuhusiana na masuala ya Kinga, huduma hii ni bure haina malipo.
Wabillah tawfiq.
Maana na dhana ya uchawi
Audhubillah mina shaitwani rajim, Bismillah Rahman Rahim, wa swalatu wa salaam ala nabiyinna Muhammad wa alihi wa swahabih.
Ama baada ya kumuhimid Allah subhannallah wa taallah na kumtakia rahma mtume wa Allah alihi na swahaba zake, niende Moja kwa moja kwenye mada. Maana na dhana ya uchawi.
Hakika jamii wakati fulani imegawanyika makundi matatu, au manne, wako naodhani nakudhani hakuna uchawi, wapo wanaofanya matendo haya ya kichawi bila ya kufahamu kwamba wanafanya uchawi, wapo wanaofanya matendo ya kichawi wakifahamu kwamba wanafanya matendo ya kichwawi, na kundi la mwisho ni lenye watu wanaofahamu uchawi upo na hawafanyi matendo haya ya kichawi kwa namna yoyote Ile, kwenye mada hii tutajadili kwa kifupi juu ya maana na dhana ya uchawi, lengo si lingine ila kuelimisha na kuleta ufahamu, na tutaegemea kwenye Qur'an tukufu, na baadhi ya hadithi za mtume wa Allah, lakini kwa uelewa zaidi tutarejea vitabu kadhaa vya wanazuoni wakubwa kwenye dini yetu.
Ama kwa dalili za uwepo wa uchawi, Allah aweka wazi ndani ya Qur'an tukufu.
Kwenye suratul (2:102) (10:78) (10:81,82) (20:67-69) (7:117-122) ( 113:1-5) aya hizo ni ushahidi tosha kwamba uchawi upo.
Sasa tuangalie maana ya uchawi biidhinillah.
Huwezi sema naenda hospitalini kupima kadha wa kadha, wakati hiyo kadha wa kadha haipo, itakuwa ni vigumu na kwenye mifumo ya nadharia ya tiba hakuna kitu kama hicho, utasema naenda pima malaria kwakuwa malaria yapo na inafahamika kwa mapana na marefu. Kwa mantiki hii ndio maana nikaona ili adhira ifahamu vyema ni lazima niletee ushahidi wa kuwepo uchawi hasa kupitia maneno matakatifu ya Allah kisha nilete maana ya uchawi.
Uchawi (sihiri katika lugha ya kiarabu matendo yanayo mhusisha shetani na kwa msaada wake ) amesema Allaithi
"Asili ya sihiri ni kukigeuza kitu katika hakika yake hadi sehemu nyingine." Al Azhay tahdhubuhllghah 4-290.
Shamir amepokea kutoka kwa Ibni, Aisha alisema, "Waarabu wameitia sihiri kuwa ni sihiri, kwa sababu huondoa uzima hadi kwenye maradhi"
Ibnu Faris amesema kuhusiana na sihiri,"watu wamesema ni kudhihirisha batili katika sura ya haki."
Uchawi katika Sheria
"Sihiri katika istilahi ya kisheria imehusika na Kila jambo ambalo sababu yake imefichika na linasawirisha kwa namba isiyo hakika yake, na huwa ikipitika kwa namna ya kuficha na kuhadaa." Fakhruddin Arrazy[Almisbahulmumir(260)]
" (Uchawi)Sihiri ni kifundo, zinguo na maneno yanayosemwa au kuandikwa , au(mtu) afanye jambo litakaloathiri katika mwili wa aliesihiriwa au moyoni mwake au akilini mwake bila ya kumshika. Nayo ina hakika, kuna yenye kuuwa, na yenye kutia maradhi, inayomzuia mtu asiweze mjimai mkewe, kuna inayotenganisha mtu na mkewe na inayomchukiza mwenza kwa mweza wake au *kuzidisha mapenzi baina yao wawili." (Almughni [10/104])/Assarim Albattar Fittassaddi lissaharatil ashrar
Tafsiri ya uchawi ni maafikiano baina ya mchawi na shetani juu kwamba atende baadhi ya mambo ambayo ni haramu au ya kishirikina katika mkabala wa shetani kumsaidia yeye na kumtii katika analotaka. Assarim Albattar Fittassaddi lissaharatil ashrar tafsri ya kiswahili Fasihinya kwanza/18 Wahid Abdussalam Bali Fasir ya Uthman M. 'Ali.
Uchawi kwa maana nyepesi ni matokeo yenye athari kwa kiumbe tokana na matendo ya siri ya kichawi.
Uchawi unaweza kuwepo na usiathiri mpaka kuwe na matendo yanayo beba uchawi huo kwa kusudio maalumu, matendo hayo ndio yanayo gawanya uchawi kwenye makundi kadha. Uchawi lazima uhusishe shetani ili uweze kutokea.
Allah atunusuru waja wake maana, kwa tafsiri hii ya uchawi nafsi zetu ni mashuhuda wa maana na nadharia ya uchawi. Allah subhannallah wa taallah ametupa Qur'an kama ponyo na rahma, ndani yake kuna suluhu ya Kila jambo, tufanye toba kwa yale yote tuliyofanya bila kukusudia ila ni kuzingwa na kadhia za maisha yetu, tumuombe mola atulinde na sheitani. Tujitahidi kufanya jitihada za kupata elimu ya msingi juu ya dini yetu humo tutapata ujuzi wa jinsi gani tunaweza kujilinda na uchawi, na jinsi gani tunaweza fanya kuondoa kadhia na athari za uchawi kwenye maisha yetu, Allah ni mjuzi wa kila kitu, ndani ya Qur'an kuna namna bora zaidi ya kujiepusha na matendo ya kichawi.
Wabillah tawfiq
Uchawi kwa mujibu wa Qur'an na hadithi
Bismillah Rahman Rahim
Kwa jaala zake Allah aliyetujalia uzima na utimamu wa nafsi na mwili, tuwaombee maghafira wazee wetu, ndugu na jamaa waliotangulia mbele za haki, lakini pia mshekh, na waalimu waliofanya jitihada kubwa mno kwa jaala zake Allah mpaka dini hii ikatufikia sisi.
Ama Leo tuangalie kwa kifupi uchawi kwa mujibu wa Qur'an na hadithi, awali tuliangalia maana na dhana ya uchawi.
Kwenye WIQAYATUL INSAN inaelezwa dalili ya uwepo wa majini na mashetani, mafungamano ni ya nguvu baina ya jini na mchawi. Majini na mashetani ndio msingi muhimili wa uchawi, kwakutokuwa na ujuzi na ufahamu wa kutosha kuna kundi la watu miongoni mwa makundi manne niliyoeleza awali kwamba linakanusha kuwepo kwa uchawi, lakini pia majini.
Sisi tunaamani katika maandiko matakatifu ya Allah subhannallah wa taallah, kwa kupitia Qur'an tukufu zifuatazo ni aya zinazoonyesha dalili za uwepo wa majini.
• Allah subhannallah wa taallah anasema: (وإذ ضرفنا إليك نفرا من الخن يتسمون القران )
" na (wakumbushe) tulipokuletea kundi la majini(kuja kwako) kusikiliza Qur'an." (46:29)
• Allah anasema
( يا معشرا الجن وانشاء الم ياتكم رسول منكم يقصون عليكم آياتي وينذرونكم يمكن هذا)
(" Siku ya qiyam wataambiwa): enyi makundi ya Majin na wanadamu! Je, hawakumufikieni mitume miongoni mwenu kukubainishieni Aya zangu na tukuonyenu mkusanyiko wa siku yenu hii ya Leo?" (6:130)
Allah subhannallah wa taallah pia amesema:( يامعشر الجن وانس إن استطعتم إن تنفذوامن أقطار السموات والأرض فانفذوالا تنفذون إلا بسلطان)
"Enyi jamii ya majini na watu! Kama mtaweza kupenya katika mbingu na ardhi, basi penyeni. Hamtapenya ila kwa nguvu zangu." (55:33)
Allah subhannallah wa taallah amesema:
(قال توحي إلي إنه استمع نغر من الجن فقالوا إنا سمعنا قران عجبا)
" Sema: imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi Moja la majini lilisikia (Qur'an): 'likasema hakika tumesikia Qur'an ni ya ajabu." (72:1)
Allah amesema:
(وأنه كان رجل من اني يعودون برجل من حال من الجن فزادوهم رهقا)
" Na hakika kulikuwa na wanaume miongoni mwa wanadamu wakijikinga kwa wanaume miongoni mwa Majin; kwa hivyo wakazidishia taklifu." (72:6)
Allah amesema:
(إنمايرد الشيطان إن يوقع بينكم العداوات والبغضاء في الخمر والميسر ويصدكم عن ذكر الله وعن الصك فهل انتم منتهون
"Hakika shaitwani anataka kuwatia uadui na bughudha baina yenu kwa ajili ya ulevi na kamari na anataka kuwazuilia kumkumbuka Allah na (kwazuilia) kuswali. Basi je mtaacha(mabaya hayo)?" (5:91)
Allah amesema:
( يا ايها الذين آمن لا تتبعوا خطوات الشيطان ومن يت خطوات الشيطان فاءنه يامر بالاحساء المنكر)
"Enyi mlion amini! Msimfuate nyayonza shetani; na atakayefuata nyayonza shetani(atapotea) kwani yeye huamrisha mambo ya uchafu na maovu."(24:21)
Allah subhannah wa taallah kupita Qur'an ameonyesha uwepo wa viumbe hawa majini, Aya ni nyingi, na ipo sura nzima inayozungumzia majini, ndani ya Qur'an neno jini limetajwa mara 22, neno majinni limetajwa mara Saba, neno shetani limetajwa mara 68 na neno mashetani limetajwa mara Saba. Kwa kukamilisha kipengele hichi tuelewe kuna Aya nyingi zimetaja majini na mashetani.
Ama ushahidi wa kuwepo majini katika Hadithi ziko riwaya kadha zinazothibitisha uwepo wa majini.
Ibni Masoud Allah amuwie radhi, amesimulia "Tulikuwa pamoja na mtume swalallah alihi wa salaam, usiku mmoja, mara tukamkosa, tukamtafuta katika majangwa na mabonde, tukasema:"ameuawa" Basi tukalala usiku mbaya waliowahi kulala watu. Kulipopambazuka mara tukamuona akija akitokea upande wa Hira. Tukamwambia: "Ya Rasuullah, tumekukosa na tumekutafuta Wala hatukukupata, basi tukalala usiku mbaya waliowahi kulala watu, Akasema:"nilijiwa na mwitaji wa majini nikaenda naye nikawasomea Qur'an." Tukaenda naye akatuonyesha athari zao na athari za mioto yao. Wakamwomba akiba. Akawaambia:"Ninyi Muna Kila mfupa uliotajiwa jina la Allah juu yake utakaoangukia mikononi mwenu wenye nyama, na Kila samadi ni chakula cha wanyama wenu." Mtume swalallah alaihi wa salaam, akatwambia :" Basi msitambe kwavyo kwani ni vyakula vya wenzenu."( Muslim[4/170])
Abdullah bin Abas Allah amuwie radhi, amesimulia, mtume swallahu alaihi wa salaam aliondoka pamoja na sahaba zake wakielekea solo la 'Ukadh, na kulikuwa kumezuiwa baina ya mashetani na habari za mbinguni na wamerushiwa vimondo, mashetani wakawarejelea jamaa zao, wakamuuliza "mnani?" Wakawaambia: " tumezuiliwa baina yetu na habari za mbinguni na tukarushiwa vimondo.' wakawaambia: ' hamkuzuiwa baina yenu na habari za mbinguni ila kuna kitu kimetokea. Safirini mashariki ya ardhi na magharibi yake na mutazame ni koi hicho kilichozuia baina yenu na habari ya mbinguni.' Basi wakaondoka wale walioelekea upande wa Tihama mpaka mtume swalallah alihi wa salaam naye Yuko Nakla wakielekea katika soko la Ukadh, naye akiwaswalisha Shaba zake swala ya alfajir. Waliposikia Qur'an, walisikika wakisema:'Wallah jambo hili ndilo lililozuia baina yetu na habari za mbinguni.' Waliporejea kwa jamaa zao waliwaambia: ' Enyi jamaa zetu, sisi tumesikia Qur'an ya ajabu, inayoongiza katika uongofu, kwa hivyo tumeiamini, Wala hatutamshirikisha yeyote na mola wetu.' Allah akamteremshia mtume wake Aya hii: "sema: imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi la majini lilisikia (Qur'an)..." (72:1). Na hakika alifunuliwa kauli ya majini"
Aisha Allah amuwie radhi amesimulia: "Mtume swallahu alaihi wa salaam amesema: "Malaika wameumbwa kwa nuru, majini wameumbwa kwa ulimi wa moto na Adam ameumbwa kwa namna muliyosifiwa." ( Ahmad [6/153,18]), Muslim (18/123 Nawawwy]).
Safiyyah Binti Huyayyi Allahq muwie radhi amesimulia: Mtume swallahu alaihi wa salaam amesema: " Hakika shetani hupitqbkwa mwanadamu mapito ya damu." (Bukhar [4/282 Fa-hi), Muslim(14/155 Nawawwy])
Abdullah bin Umar Allah amuwie radhi amesimulia: "Mtume swalallah alaihi wa salaam amesema:"Anapokula mmoja wenu , ale kwa mkono wake wa kulia, na anapokunywa anywe kwa mkono wake wa kulia, hakika shetani anakula kwa mkono wake wa kushoto na anakunywa kwa mkono wake wa kushoto." (Muslim[13/191 Nawawwy])
Abu Huraira Allah amuwie radhi, amesimulia: Mtume swallahu alaihi wa salaam amesema:"yeyote anaye zaliwa hudukuliwa na shetani, akapiga ukelele kutokana na mdukuo wa shetani, ispokuwa mwana wa Maryam(Nabii Isa) na mama yake" (Bukhari [8/212 Fati-h) na Muslim( 15/120 Nawawwy])
Abdullah bin Mas'ud Allah amuwie radhi amesimulia: " mbele ya mtume swalallah alihi wa salaam kulitajwa mtu alielala usiku mpaka akapambazukiwa. Akasema:"Huyo ni mtu amabe, shetani amemkojolea masikioni mwake."(Bukhari[3/28 Fat-hi) na Muslim (6/64Nawawwy)
Abu Qadada Allaha amuwie radhi amesimulia:"Mtume swalallah alihi wa salaam amesema: " Ndoto njema yatoka kwa Allah, na njozi yatoka kwa shetani. Basi atakaye ota kitu kinachomchukiza, ateme upande wake wa kushoto mara tatu na ajilinde kutokana na shetani; kwani haitamdhuru." (Bukhari[12/283 Fat-hi]na Muslim (15/16 Nawawwy)]
Abu Said Al- Khudry Allah amuwie radhi amesimulia: " Mtume swalallah alaihi wa salaam amesema " Atakapoenda mwayo mmoja wenu, azuie kwa mdomo wake kinywani mwake; hakika shetani huingia (asipoziba)." KMuslim[18/122 Nawawwy]) na Darimy (1/321)]
Hadithi hizi zinatosha kwa anayetaka kufahamu na kuwa na hakika. Pasipo na shaka imetubainikia kwa msingi wa Qur'an tukufu na Hadith kuwa mashetani ni hakika wapo ispokuwa kwa mtu anayeshindana na haki, anayefuata hawaa za nafsi yake pasipo uongofu utokao kwa Allah.
Kwa upana zaidi juu ya maudhui haya, yanapatikana katika kitabu "WIQAYATUL INSAN, MINALJINNI WASHAITAN"(Kinga ya mwanadamu dhidi ya majinni na mashetani).
Wabillah tawfiq
Usafi wa mwili na nafsi
Assalam aleikum warahamatullah wabarakatuh
Kwenye somo ili tutaangalia kwa kifupi biidhinillah kuhusiana na usafi wa mwili na nafsi, hapa hatuzungumzii mambo matano muhimu kuhusiana na usafi "hamsun minal fitirat" la hasha tunachozungumzia hapa ni usafi ambao sharia ya fiqih imeweka bayani kwamba muislam hataweza fanya ibada mpaka awe kwenye hali hizi, maelezo ni mengi, hatuwezi yasema yote hapa. hili limethibiti kwenye Qur'an na Sunna,
Tujifunze pia kuhusu janaba, najisi na kadhalika, tujifunze hali nyingine ambazo zinaweka kizuizi kwa mja kutofanya ibada, hapa Niko mbali kidogo na hali za kimaumbile kama ada kwa akina mama nakadhalika.
Mfano, kunywa bombe na kamari haya huondoa uimara wa nafsi ya mja kwenye utambuzi, udhaifu wa maamuzi, umakini heshima na adabu mbele za Allah, humuweka mja mbali na neema za Allah na baraka ya kufanya ibada na kumpwekesha Allah (5:91)
Allah atunusuru, na tuzidi kumuomba imani zetu ziimarike, atujalie hamu ya kujifunza elimu ya dini yetu na kuhifadhi vyema ili tutekeleze maamrisho na makatazo vizuri wakati tunapofanya ibada mbalimbali, ajalie tuwe wasafi wa miili yetu na nafsi pia.
Tafadhali wasiliana nasi ili kupata maelezo zaidi kuhusiana na usafi wa mwili na nafsi kupitia alternative hub.com, elimu hii ni bure haina malipo.
Wabillah tawfiq.
Dalili hizi huashiria kuwa kuna uchawi ndani ya mwili.
Assalam alaikum warahamatullah wabarakatuh.
Tunamshuru mwenyeezi mungu kwa kutujalia afya njema na utimamu wa akili na mwili, kwa wale wenye hali ya ugonjwa na matatizo mbalimbali, tunawaombea kwa Allah wapate nafuu na kupona kabisa.
Zifuatazo ni dalili zinazoashiriq kwamba kwenye mwili kuna uchawi.
* Uchovu kupindukia.
* Kuhisi maumivu pasipo na sababu.
* Kutoka mapaka meusi amabayo na Kila Kila jitihada za kuyaondoa kwa dawa mbalimbali hushindikana.
* Kuwa muoga kupindukia.
* Kuweweseka usiku.
* Kuwashwa mwili.
* Kuamka hukunumelishwa kitu.
* Kutofanikiwa kwenye shughuli au biashara, ingawa unafanya ibada na unaomba sana.
* Kutopata kazi ingawa unavigezo vya kupata kazi.
* Kutopata ujauzito, wakati mwili uko sawa na hakuna tatizo la kibaiolojia.
* Kukimbiwa na wachumba, migogoro katika ndoa isiyo na sababu, pesa kupotea.
* Kuumwa mara kwa mara, japo unatumia dawa za hospitali lakini maradhi hayaponi.
* Kusemwa vibaya hata ukifanya wema.
* Kuwa na hasira bila sababu.
* Ndoto za kuogofya, ugomvi, makelele, kupigana, kupaa, kufukuzwa n.k
Hizo ni miongoni mwa dalili zinazoashiria kwamba kuna uchawi kwenye mwili. Allah atujalie tufanye jitihada za kujilinda kwake dhidi ya uchawi na watumishi wake, wasiliana nasi kuondoa changamoto hizi na nyinginezo bi idhinillah.
Wabillah tawfiq.
Aya za kubatilisha uchawi
Assalam alaikum warahamatullah wabarakatuh
Waswalatul wa salam ala nabiyyina Muhammad wa alihi wasabihi kama swailaita wa barakta ala Ibrahimma Wala alihi.
Tunamshuru mwenyeezi mungu kwa kutujalia afya njema na utimamu wa akili na nafsi.
Zifuatazo ni miongoni mwa aya zinazobatilisha uchawi, kama mja amerogwa atakaposomewa Aya hizi iwapo kuna jini aliyeingia kiuchawi kwenye kiwiliwili chake atahangaika sana na hata kulia.
((وأحيانا إلى موسى أن ألف عصاك فاءذا هى تلقف ما يأفكون ))
،((فوقع الحق وبطل ما كانوا يعملون))
((غغلبوا هناك وانقلبوا صغرين))
((وألقى السحرة سدين ))
((قالوا ءامنا برب العلمين))
((رب موسى و هارون ))
Suratul Araf 117-122
((فلما ألقوا قال موسى ما خيتم به السحر إن الله سيبطله إن لله لا يصلح عمل المفسدين ))
((و يحق ٱلله الحق بكلمته ولو كرة ٱلمخرمون))
Suratul Yunus 81-82
((والف ما فى يميبك تلقف ما صنعوا إن ما صنعوا كيد سحر ولا تفلح الساحر حيث أتى))
Twaha 68
Kwa haya na mengine mengi wasiliana nasi kupitia njia za mawasiliano tulizo orodhesha.
Wabillah tawfiq
Masharti ya kusoma Rukya
Assalam alaikum warahamatullah wabarakatul.
Wasalatu wa salaam ala sayyidina Muhammad wa alih waswahabih kama barakta waswalaita ala sayyidina Ibrahima wa alih waswabih wasalam.
Miongoni mwa vitu vinavyo utambulisha uislam iko pia njia ya matibabu inayofuata, japo wako baadhi miongoni mwetu wanadai haikuthibiti na Hadith inayohusiana na njia hizi ni dhwaifu, lakini ingekuwaje kama njia hizi Bora kabisa zisingekuwepo?
Tumepata kueleza kwa kirefu zaidi kwenye makala zilizotangulia, kwa kupata elimu juu ya suala Hilo.
Leo tuangalie masharti kwa msomaji wa Rukya.
Lakini awali ya yote tutambue ya kwamba hakuna degree ya mtu kuwa Raq.
Kinachotakiwa, awali ya yote ni mtu huyu ajitenge na maasi na awe mwenye kutenda mema.
Afuate Sunna za mtume Muhammad swalallah alaihi wa salaam, awe ni mwenye kusoma Qur'an, kufunga Sunna, kutoa sadaka, awe mtoaji wa daawa kuhusu athari za mashetani duniani na akhera wa wagonjwa wake, ajiepushe na batili na aidhihirishe Haki, asipende kupiga domo, awe mcha mungu, maswarti anayompa mgonjwa yeye ayatekeleze kwa kuyaishi, asihisi yeye ni mjuzi ila amtegemee Allah na atagemee msaada wa Allah, ajitenge na maasi yote kwani ametangaza vita na viumbe waliomzidi uwezo na asiowaona.
Pia atambue majini wote wanaotoka bila kusilimu ni maadui kwake na watafuata nyendo zake kwa takribani siku tisini baadae ya kutolewa.
Ajikinge na shetani na majini waovu kwa kusoma azkar za asubuhi na jioni.
Tumuombe mwenyeezi atulinde na shari za majini na binaadamu waovu, atujalie afya njema na atuepushe na shari za nafsi zetu.
Kwa maelekezo zaidi wasiliana nasi kupitia njia za mawasiliano zilizo arodheahwa kwenye website hii.
Wabillah tawfiq.
Jini kisigo
Assalam alaikum warahamatullah wabarakatul.
Allahumma swali ala sayyidina Muhammad wa alih waswabih, kama barakta waswalaita ala sayyidina Ibrahima wa alih.
Umepata kusikia jinni huyu Ghwwashi?
Jioni huyu hupendelea kukaa katika mabahari, chemichemi na kwenye moto.
Dalili za jinni huyu kwenye kimwili ni hizi zifuatazo:
- Kuwashwa mwili na kutoa malengelenge panapowashwa.
- Kuvimba sehemu za mwili kama vile uso nakadhalika.
- Kutokuwa na madonda mdomoni ambayo hayaponi hata baada ya kutumia dawa kadha za hospitali.
- Mwanamke kuwashwa matiti na kutoka madonda sehemu za Siri.
- Mwanamke kutokuwa maziwq hata kama hanyonyeshi.
- Kwa mwanaume kuvimba dhakari au kusisinyaa.
Dalili ni nyingi zaidi la hizi zilizoorodheshwa tutosheke kwa hizi chache.
Ziko sababu pia zinazopelekea jini huyu aingie kwenye kiwiliwili Cha mja.
- Watoto wadogo wamekuwa na tabia ya umri ya kwenda kwenye vyanzo vya maji kama vile chemchem na kuanza kucheza humo.
- Kuogelea kwenye bahari, maziwa na moto pasipo kutaja jina la Allah.
- Kufanya vitendo vya hivyo na kupiga kelele wakati wa kuogelea.
- Kuingia kwenye makazi ya majini haya humo majini.
- Mwanamke kuogelea uchi au kukaa pendozoni mwa maji, mtoni, baharini, ziwani.
Namana ya kumtibu au kumtoa jini huyu.
Matibabu ya kumtoa jini huyu yanalingana na yale ya kumtoa jini Ashq, tumia fusho la miski.
Ikumbukwe majini haya waovu hawapendi harufu nzuri ila baya, kwahiyo tumia miski nyeupe na nyeusi ziwe za maji.
Na utapaka kwenye sehemu 32 mwilini.
SWALA
Assalaam aleikum warahmatullah wabarakatuh, ndugu zangu miongoni mwa nguzo Tano za Uislam ni SWALA, hivyo nimeonelea kukumbushia baadhi ya mambo ya muhimu kuhusiana na nguzo hii adhwimu.
Kwanye kurasa hizi na panapo majaliwa ya Allah tutaangalia kwenye Cheo Cha swala na hukumu zake mambo yafuatayo.
- Maana ya swala.
- Hadhi ya swala katika Uislam.
- Utukufu wa swala
- Hukumu ya swala.
- Swala Ina mlazimu nani?
- Hukumu ya mwenye kuacha swala.
Swala kilugha
Swala kilugha ni "Maombi"
Swala kisheria
Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu عزاوجل na kwa maneno na vitendo maalum, vinanavyoanzia kwa takbiri na kumalizika kwa kupiga salam.
Hadhi ya swala katika Uislam
1. Swala ni nguzo ya pili katika Uislam.
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Uislam umejengwa juu ya nguzo Tano, kukiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kuwa hapana mola apasee kuabudiwankwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja na Mtume wake, na kusimamisha Swala ¹
2. Swala ndoto amali Bora kimatendo. Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu صلى الله عليه وسلم (Amal bora kuswali mwanzo wa wakati)
3. Swala ni upambanuzi baina ya Uislam na ukafiri. Mtume صلى الله عليه وسلم amesema( Baina ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha swala)²
4. Swala ni nguzo ya Uislam. Juu yake baada ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu ndio ya jenga Uislam. Mtume صلى الله عليه وسلم (kichwa Cha jambo hili ni Uislam na nguzo yake ni Swala)³
¹imepokewa na Muslim
²imepokewa na Muslim
3.imepokewa ana Ahmad Tutaishia kwenye nukta hii, panapo majaliwa ya Allah subhannah wa taalah tutaendelea na sehemu ya pili ambayo, ni Fadhila za swala.