Matibabu ya kisheria, Dua mbalimbali na dawa za kisunna

Matibabu ya kisheria, Dua mbalimbali na dawa za kisunna

Karibu

Dua na matibabu

Blackseed has a healing power over many diseases and conditions except death

Blackseed has a healing power over many diseases and conditions except death

Kuondoa majini na uchawi kwenye mwili wa binadamu

Assalam alaikum warahamatullah wabarakatuh

Shukran ni zake mwenyeezi mungu aliye tujalia uhai na afya njema na kutujalia wengi miongoni mwetu akili timamu na  utambuzi wa baya na jema.

Rehema na amani zimuendee nabiya alihi na swahaba zake.

Miongoni mwa shida zinazo mkabili mwanadamu, ni majini na uchawi, madhara mengi yamekuwa yanatukumba kutokana na kuvamiwa na majini na uchawi kwa namna mbalimbali, wachawi hushirikiana na majini kwa makubaliano kufanya dhulma hii, au wakati mwingine majini huvamia wanadamu na kuwadhiru.

Ziko njia nyingi za kuondoa majini na uchawi kwenye mwili wa binadamu. Kwenye ukurasa huu tutangalia njia miongoni mwa nyingi zitumikazo, nazo ni kwa kutumia dawa za kisunna, hii ni kwasababu kumkabili jini au uchawi kunaweza leta madhara ya moja kwa moja kwa (tabibu) au mgonjwa kama kiwango cha uchamungu ni cha chini, kwa rehma zake Allah kwa kutumia dawa hizi jini au uchawi utatoka In Sha Allah. 

Dawa hizi zimegawanyika kwenye makundi matatu, ziko za kufukiza, kunywa na kupaka au kuoga.

Dawa za kufukiza ni hizi zifuatazo.

1. Pakanga 

2. Pachori 

3. Nanaa 

4. Habbatsoda 

5. Binzari nyembamba 

6. Kaafuri(karafuu maiti)

7. Giligilani 

8. Takataka za baharini 

Dawa hizi zinapatikana kwenye maduka ya dawa za kisunna, baada ya kuzikusanya, hatua inayofuata ni kuzitwanga kwa pamoja mpaka zitakapokuwa unga.

Dawa hizi nizakujifukiza, kwa hiyo mtu aliye athirika na jini/majini au uchawi atasaidiwa kufanya zoezi hili, afunikwe shuka, mbele yake yawekwe makaa ya moto, kisha dawa hii itawekwa kwenye moto, kipimo ni kijiko cha chai, Moshi utakao toka ndio dawa, mgonjwa atakaa kwa muda wa dakika tatu mpaka tano, nguo atakayofunikwa au kujifunika isiwe nzito sana, inatakiwa iwe na uzito wa khanga nyepesi. Wakati zoezi linaendelea kuna mambo kadha yanaweza kutokea, mgonjwa kutapika, kuweweseka na wakati mwingine jini alilosubiwa nalo au kumkumba kupanda kwa namna kadhaa, kuleta kejeli, kiburi na majigambo, lakini pia vurugu na vitisho.*** Kwenye Somo lijalo tutaezea nini cha kufanya kama hali hizi zitatokea, lakini  jini aliyesibiwa anaeza kupanda nakuaga kwamba anaondoka au uchawi kubatilika.

Mgonjwa atatumia dawa hizi mfululizo kwa muda wa siku saba, asubuhi na jioni.

Namna ya pili ya kumsaidia mtu aliyeingiwa na majini na uchawi, ni kupitia dawa za kupaka, dawa hizi zinatakiwa zitumike kipindi hizo za kufukiza zinatumika. Nazo nazo zitatumika asubuhi na jioni kwa muda wa siku Saba.

Dawa hizi ni:

1. Mafuta ya kitunguu saumu 

2. Mafuta ya zeti 

3. Miski ya unga(nyeupe)

Dawa hizi zinachanganywa kwenye chombo kimoja, kama chupa basi liwe lenye uwezo mkubwa ili kuweza kuingia dawa zote, ikiwezekana ujazo wa Kila dawa uwe milliliters 300, weka kwenye chombo husika Kisha changanya dawa hizi.

Kama nilivyosema awali dawa hizi niza kupaka, hivyo mgonjwa anatakiwa afuate maelezo haya, anatakiwa apake kwenye ncha za vidole vya mikono na miguu,(kwa mwanamke na kwenye chuchu za mazima)

Lakini kwenye maeneo yafuatayo:

1. Tundu za pia 

2. Tundu za masikio 

3. Kwenye tupu zote mbili 

4. Kwenye kinena 

5. Midomo 

6. Kwenye mapaja sehemu za ndani.

Dawa hizi mgonjwa ajipake yeye mwenyewe. au kwa mwanamke atapakwa na mume wake.

Dawa ya mwisho ni Sanamaki, haya ni majani tiba yanayopatikana bara Arab na Asia.

Majani haya kiasi cha vijiko saba vya chakula, utaweka kwenye maji lita moja na nusu, yatachemshwa mpaka walau robo Lita iwe imepungua kabisa, itaipuliwa na kuachwa ipoe kabisa, kisha utachukuliwa asali mbichi robo Lita, asali hii itawekwa kwenye dawa Ile iliyoachwa ipowe na kuchanganywa. Kisha dawa hii sasa itasomewa Rukya ya kisheria, kama mtu hawezi basi atafutwe mtu anayeweza kusoma Qur'an vyema. Kipimo cha dawa kwa matumizi ni nusu ya kikombe cha chai nasi vinginevyo, anywe kiasi husika asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba.

Mgonjwa anatakiwa atumie dawa hii kwa muda sawa na atakavyokuwa anatumia dawa mbili zilizoelezwa tayari, lakini pia dawa hii inaweza pia lainisha tumbo, hiyo mgonjwa anaweza pata hali ya kuharisha  kama ikizidi anywe maji ya baridi kuzuia hali hiyo.

Kwa maelezo zaidi juu ya utaratibu na matibabu haya, wasiliana nasi kupitia njia za mawasiliano zilizoorodheshwa.

Wabillah tawfiq 



"Musa akasema:"Mnasema juu ya haki ilipowajia? Huu ni uchawi? Na wachawi hawafaulu."(10:77)

Kubatilisha uchawi

Assalam alaikum warahamatullah wabarakatuh, waswalatul wa salam ala nabiyyina Muhammad wa alihi wasabihi wa salaam. Ama baada ya kutaka rehma na amani toka kwa Allah subhannallah wa taallah na kumsaalia mtume wetu alih na sahaba zake, mambo haya baadhi ya nyakati hutia hofu kwenye nyoyo zetu, ubora ni kufahamu miundo, mitego, namna, jinsi na muunganiko wawatumishi, madhara na gharama za uchawi. Ni vyema kuwa na ufahamu wa mambo haya kuliko kupambana na adui usiye mjua hata kidogo, lakini elimu ni akiba isiyo oza, kupitia elimu ya aina hii ya matibabu itakusaidia sasa kufahamu ni nani unayemkimbilia pale unapopatashida.  Kubatilisha maana yake ni kuondoa, na hapa tunazungumzia uchawi, hivyo tutaangalia namna kadha wa kadha, njia mbalimbali za kuondoa mathara ya uchawi wa aina mbalimbali. Lakini pia kwenye fasihi hii na nyingine zinazohusiana na tiba, tutakuwa na mambo ambayo hayakudhihiri kwa waja kutoka kwa mtume wa Allah swalallah alaihi wa salaam katika kutibu hali fulani, lakini yapo katika kawaida ya jumla ndani ya Qur'an na Sunna. Kwa mfano utakuta tiba ya Aya moja ya Qur'an au nyingi kutoka sura mbalimbali, basi yote haya yapo chini ya kauli yake Allah "Na tunateremsha katika Qur'an ambayo ni ponyo na rehema kwa wanaoamini" (17:82). Katika ulamaa muna wasemao kuwa: ' makusudio ya ponyo ni ponyo la kimaana - yaani kutokana na shaka, shiriki, ufuska na ubaya.' Na kuna wasemao kuwa makusudio ni ponyo la kimaana na kihisia. Na kuna dalili nyingine zilizo wazi kuliko hii, bali ndio tegemeo katika mlango huu, Aisha Allah amuwie radhi, amesimulia: "Mtume swalallah alaihi wa salaam aliingia kwake na kuna mwanamke aliyekuwa akimtibia (Aisha) na akimzingua, Mtume swalallah alaihi wa salaam akamwambia "mtibu kwa kitabu cha Allah." (Imetefsriwa na Albany katika Silsilatus Sahihah [1931]) Kutokana na hadithi hiyo, kuna uhakika kwamba mtume swalallah alaihi wa salaam amejumlisha Qur'an yote na si aya maalum au sura maalum, basi ikawa bayani, Na katika majaribio ya kimatendo ikabainika kuwa Qur'an yote ni ponyo. Na hakika Qur'an sio tiba ya uchawi tu bali ni tiba hata kwa maradhi ya viungo pia.

Anaweza mtu akaleta fikra ya kwamba, ili pawe na uhakika kwamba ni vyema pawepo dalili kwa aya hizi za Qur'an kutibu mgonjwa, au tutasimama mpaka tupate nasi (maandiko) thabiti kuwa mtume swalallah alaihi wa salaam alizingua mtu kwa Aya hii kwa ugonjwa huu. Watu wa aina hiyo waelewe bayana kwamba mtume wetu Muhammad swallahu alaihi wa salaam aliweka kawaida ya ujumla katika zinguo. Imedhihiri katika Sahihi Muslim kuwa walisema " ya rasuulallah, hakika tulikuwa tukizinguana zama za ujahilia. Akasema  "Nileteeni zinguo lenu (nilitizame) Zinguo halina ubaya madamu halijakuwa na shiriki."(14/187 Nawawwy)]

Kwa hadithi hii basi inajuzu kuzingua kwa Qur'an, Sunna, Dua na mengineyo.

Kwa muhtasari huo sasa tuangalie sehemu ya kwanza ambapo tutaangalia jinsi ya kubatilisha uchawi wa kufarakisha.

Allah amesema katika suratul Bakarah  

"Wakafuata yale waliyofuata mashetani, (wakidai kuwa ) katika ufalme wa (Nabii) Suleiman; na Suleiman hakukufuru, Bali mashetani ndio waliokufuru, wakiwafundisha  watu uchawi (waliokuwa wakiujuwa wenyewe tangu zamani), na (uchawi) ulioteremshwa kwa malaika wawili, Haruta na Maruta, katika (mji) wa Babil. Wala (malaika hao) hawakumfundisha  yeyote mpaka wamwambie:"hakika sisi ni mtihani (wa kutazamwa kutii kwenu); nasi msikufuru. Wakajifunza kwao ambayo kwa mambo hayo waliweza kumfarikisha mtu na mkewe (na mengineyo) Wala hawakuwa wenye kumdhuru yeyote kwayo ila kwa idhini ya Allah. Na wanajifunza amabayo yatawadhuru Wala hayatawafaa. Na Kwa yakini wanajua kwamba aliyekhiari haya hatakuwa na sehemu yoyote katika akhera. Na bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia( starehe za ) nafsi zao (za akhera). Laiti wangelijua, (hakikawasingefanya hivi)." (2:102,103]. 

Jabiri Allah amuwie radhi amesimulia: " mtume swalallah alaihi wa salaam amesema : " Hakika ibilisi hukiweka kiti chake juu ya maji, Kisha akavituma vikosi vyake. Basi mwenye cheo Cha karibu naye zaidi ni yule mwenye fitina kubwa zaidi. Mmoja wao huja na kusema: nimefanya kadha wa kadha.' yeye humwambia: 'hujafanya kitu!' Kisha huja mwingine Akasema: ' sikumwacha(mwanadamu) mpaka nimemfarakisha yeye na mkewe.' hapo humkaribisha kwake na akimwambia: wewe ni askari mzuri sana!' Al-a'mash amesema: "Nadhani alisema "...basi Huwa naye." (Muslim[17/157])

Naam, kwa jaaza zake Allah subhannallah wa taallah, tutaeleza kwa kifupi aina hii ya uchawi na aghalabu mifano mmoja wa jinsi mchawi anavyofanya, Kisha tutaelezea tiba yake.

Kwanza kufarakisha hukunhuelekezwa kwenye mafungamano imara, mahusiano yaliyo dhabiti. Mtu na mkewe, mtu na baba yake, mtu na nduguye, mtu na rafikiye, mtu kufarakisha baina ya mtu na mshirika wake katika biashara au jambo lingine. Kufarakisha mtu na mkewe aina hii ya kufarakisha ndiyo hatari zaidi na ndiyo iliyo sambaa sana.

Zipo dalili kadhaa zinazobainisha mtu amekumbwa na uchawi huu.

•kubadilika kwa hali ya upendo na mapenzi na kuwa bughudha.

•sababu ndogo kukuzwa na kuwa kubwa. 

•kutoa udhuri usio na maana kwenye  jimai. 

•mtu kumuona mwenza kwenye taswira tofauti. Wakati mwingine ya kuogofya. 

•Aliyekumbwa na uchawi huu huchukia Kila kitu kinachofanywa na mwenzake haijalishi mambo mema au la.

•Anapokuwa mbali humkumbuka na kuwa na hamu ya mwenzake lakini akiwa karibu uhisi dhiki kubwa ya nafsi.

Aina hii ya uchawi hutokeaje??

Mtu huenda kwa mchawi kwa dhumuni la kufarakisha wahusika, baada ya hapo hutumwa adhari ya muhusika, kama vile alipo kanyaka kwenye mchanga, mabaki ya chakula, nyuzi za nguo, nywele nakadhalika.

Lakini pia kama si hivyo kuna njia nyingine za kufarakisha mbaya zaidi na kuna baadhi ya nyakati hupekea madhara makubwa hata vifo.

Mchawi hutoa aina ya uchawi na kumwambia muhitaji akamwage kwenye njia anayo pita anayetakiwa kufarakisha maji fulani, na baadhi ya vitu vingi mno.

Hapa nitoe ushuhuda wa wachawi, wenye msiba wa mtu muhimu sana kwenye maisha yetu,  mtoto wa kaka yetu aliwakamata maajuza wawili walioingia kwenye chumba alichoandaliwa Al maruhumu, Allah subhannallah wa taallah amsamehe yeye na sisi makosa, na amjalie yeye na mwenza wake makazi mema, na awali makaburi Yao yawe viwanja miongoni mwa viwanja vya peponi.) Waliingia kuchukuwa athari kadha wa kadhaa, sijui wengeondoka nazo nini kingetokea Allah ya alam. Kinacho muepusha mja na madhara ya mitego hii ni nyiraji na azkar mbalimbali za asubuhi na jioni 

Tiba kubatilisha aina hii ya uchawi ziko nyingi.

Awali ni lazima aliye athirika akubali mazingira ya tiba ya sharia ndio tiba sahii ya kutatua tatizo lake. Kwahiyo awamu ya kwanza ya tiba ni kukiri kwamba Allah peke yake ndiye anaye weza kuondoa tatizo alilo nalo. Akubali halinya usafi wa mwili wake, nafsi na mahala panapofanyiwa tiba.

Tiba hii Niya kisharia hivyo basi, pasiwepo ujinga, ukaidi na uhalifu wa Sheria.

Kabla ya tiba mgonjwa ni lazima apate mawaidha juu ya halibyake na halibyake baada ya tiba.

Pia mgonjwa ataulizwa maswali maalum, kuhusiana na hali yake, na Yale anayohisi kama ni mume au mke.

Mgonjwa kama ni mke matibabu yafanyike wakiwepo watu wengine, ahifadhi hijab asiwe na manukato, mafuta uzuri, na anatakiwa awe amevaa nguo za kisharia 

Sehemu ya pili ni tiba 

Mgonjwa atasomewa huku awekewa mkono juu ya kichwa chake, litasomwa zinguo sikioni mwake. Zinguo hili ni aya maalum za Rukya, zitasomwa mara tatu mutawalia, na huenda shetani aliyetumwa akapanda, in Sha Allah kwenye Somo lifuatalo tutaendelea na hatua nyingine Toka hapa tulipo ishia.

Kwa shida hii na nyingine wasiliana nasi kupitia kwa maelekezo, ushauri na tiba maalum kuondoa faraka kwenye ndoa, mahusiano nyumbani baina ya watoto na wazazi, marafiki na sehemu ya kazi.

Wabillah tawfiq 


Allah atujalie sote tuifuate Qur'an na Sunna za bwana Mtume Muhammad swalallah alaihi wa salaam

Allah atujalie sote tuifuate Qur'an na Sunna za bwana Mtume Muhammad swalallah alaihi wa salaam

Muhimu

alternative hub.com inakukaribisha kwa utatuzi wa masuala mbalimbali ya kimwili na kiroho, alternative hub au Markaz badil haishughuliki tu na matatizo mbalimbali ya maradhi yatokano na uchawi,  lakini pia mfumo wa maisha kiujumla, kibaiologia na kifikia, pia ushauri kwenye masuala kadha wa kadha kwa kuzingatia Sheria za kiislam Fikih, kwa mujibu wa Qur'an tukufu na sunna za Mtume Muhammad swallahu alaihi wa salaam, miongoni mwa vipengele tunavyotoa ushauri ni mambo gani mzazi anapaswa kufahamu anapotaraji kufanya hakika kwa mtoto wake, tunatoa maelezo juu ya zaka na tofauti kati yake na sadaka, tunatoa ushauri wa mzazi kutafuta shule bora zaidi kwa mtoto ambaye anaonekana kuwa anamtihani wa kuelewa vyema masomo yake, tunazungumza na vijana walio kata tamaa tokana na ufinyu wa ajira, hivyo tunawapa maelekezo ya jinsi gani wanaweza kutafuta jambo la kufanya. Tunashughulika na vijana waliopata mtihani wa kutopea kwenye ulevi na uraibu, tunazungumza nao, tunatoa maelekezo na hata kutoa huduma ya Dua na matibabu kadiri Allah subhannallah wa taallah alivyotujalia. Mwisho alternative hub.com au Markaz badil inatoa elimu juu ya masuala mbalimbali ya kidini, hili ni Moja kati ya masuala ya muhimu na msingi. Panapo majaliwa ya Allah hivi karibuni tutaanza kutoa majarida mbalimbali ya kielimu yasiyofungamana na madhahabu yoyote Bali Qur'an na sunna za bwana Mtume Muhammad swalallah alaihi wa salaam.

Wasiliana nasi kupitia njia za mawasiliano zilizotolewa kwenye website hii. Tunachoomba kutoka kwako ni kushirikisha (share) website hii kwa ndugu, jamaa na marafiki. Kumbuka tunatoa matibabu kwa gharama inayolingana na tatizo la mja, hakuna gharama za ziada. Matibabu yanayotolewa ni Dua, visomo mbalimbali, na dawa za kisunna, hakuna ramli.

Wabillah tawfiq.


Qur'an

Qur'an

Liondoe hili.

Assalam alaikum warahamatullah wabarakatuh.

Kwa idhini yake Allah subhannallah wa taallah Leo tunaglie kwa ufupi matibabu ya kumuondoa kwenye kiwiliwili cha binadamu jini aitwaye KISIGO/GHAWWASWI. huyu hukaa baharini, kwenye mito, visimani na hata kwenye chemchem.

Dalili za kuwa mtu amepatwa na jini huyu ni, kuvimba uso au kiuno chochote na huwa hakuambatani na maumivu.

Kuwashwa mwili na wakati mwingine palipokunywa hutoa lengelenge. 

Aliye athirika atapaka miski nyeupe na nyeusi ziwe za maji akikosa za maji achanganye miski hizo nyeupe na nyeusi kwenye umbo la unga na mafuta ya Zaituni na mafuta ya habbat saudai. Mchanganyiko huu unapakwa kwenye ncha za vidole vya mikono na miguu, matundu ya pua, matundu ya masikio, kwenye kope za macho, kwenye midomo, kwenye matiti, kwenye tundu ya mbele na nyuma ( duburi/ dhakari/farji.) Kwa muda wa wiki nne mpaka sita, Kwa jaala zake Allah jini huyu atatweza nguvu na kuondoka kwenye mwili wa aliye athiriwa na jini huyu. 

Tumuombe Allah atuepushe na madhara ya sheitwani, atuhifadhi na atulinde.

Kwa msaada zaidi wasiliana nasi juu ya tatizo hili na mengineyo.

Wabillah tawfiq.

Dawa ya maumivu ya viungo na kupooza. Dawa ya kusafisha mwili, kuondoa nuksi, mikosi na mabalaa

Dawa ya maumivu ya viungo na kupooza. Dawa ya kusafisha mwili, kuondoa nuksi, mikosi na mabalaa

Kwa matibabu ya kusafisha mwili dhidi ya nuksi, mikosi na balaa, maumivu ya viungo na kuweka sawa viungo vilivyo pooza.

Kuna baadhi ya nyakati huwa tunakumbana na shari nyingi, shari hizi hupelekea kuathirika kimwili na kiroho, uchawi,  vijicho vya shetani huleta mikosi, nuksi, na balaa, kupata maumivu makali ya viungo na hata kupooza, dawa hizi mbili ni suluhisho kwa dhiki na taabu zinazotokana na vitimbi vya majini na uchawi. Dawa zote zimefanyiwa Visomo vya Ruqia ya kisheria.

Ghasila

Ghasila

GhasilaDawa bora zaidi kutoka ALTERNATIVE HUB.COM

Dawa hii inatumika kusafisha mwili, nyumba,  mashamba, eneo la biashara, na vyombo vya usafiri.

Aswila'a

Aswila'a

Dawa maalum na bora zaidi kutoka ALTERNATIVE HUB.COM

Dawa hii ni pacha ya dawa iliyotangulia Ghasila, baada ya kuoga dawa ile, utatumia dawa hii kujipaka uso na mkono, dawa hii kwa jaala zake Allah itarudisha mvuto wako wa asili mahala pale, dawa hii itarekebisha mambo kadha wa kadhaa. Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi kipitia namba zifuatazo

+255686872507

X
This site uses cookies to offer you a better browsing experience.
You can accept them all, or choose the kinds of cookies you are happy to allow.
Privacy settings
Choose which cookies you wish to allow while you browse this website. Please note that some cookies cannot be turned off, because without them the website would not function.
Essential
To prevent spam this site uses Google Recaptcha in its contact forms.

This site may also use cookies for ecommerce and payment systems which are essential for the website to function properly.
Google Services
This site uses cookies from Google to access data such as the pages you visit and your IP address. Google services on this website may include:

- Google Maps
- Google Fonts
Data Driven
This site may use cookies to record visitor behavior, monitor ad conversions, and create audiences, including from:

- Google Analytics
- Google Ads conversion tracking
- Facebook (Meta Pixel)